Kabila lolote ulimwenguni,
hutokana na mambo mane (manne) yakiwemo jadi, Kazi, mji na sifa za watu. Na
upande mwengine nayo lugha hutokamana na mazingira maalum ya watu na utamaduni
wao. Ikiwa kabila ni desturi na mila za
watu, au ni watu walofungamana na kuwa na tabia na nyendo ambazo
zitawatofautisha wao na watu wengine, basi waswahili wana mila zao na desturi
zao kama makabila mangine(mengine) ulimwenguni. Kama kwenye maingiliano ya
kibinadamu k.m ndoa, majina, itikadi za pepo na kadhalika, basi liko kabila la
waswahili lenye mambo kama hayo.
Kabila la waswahili, utamaduni
wao, na lugha yao hupatikana ile sehemu y anti (nchi) iliyopatikana na maji ya
pwani na mwambao wa Afrika mashariki. Wenye urefu wa kilomita 1500 pamoja na
visiwa vilivyopakana na mwambao wenyewe.
Kiswahili ni lugha iliyotapakaa na kujulikana kote ulimwenguni na hata
kuliko lugha nyengine yoyote ya Afrika.
Kuna rai kuwa neon “waswahili”
lilitokea pale Muhammad Bin Abdallah Ibn Batuta na wasafiri wenzake walofika miji
ya mwambao mwaka 1331 B.K. na kummuliza kijana wa kingozi, “Man ha ulaii”? kuwa
wao kina nani? Akawajibu sisi ni As- Sawahili yaani wenyeji wa pwaa hizi. Sahil ni neon la asili ya kiarabu na wingi
wake sawahil yaani pwani (upwa) na watu wa bara arabu wakakwita huku Al-Sahili
au as-sawahiliyy na wengine hudai neon “waswahili” latokana “wa-ziwa-hili”
Lakini kabla ya ya kuja ibn
Batuta watu hao walikuwa wakiitwa wangozi, kutokana na mapokezi ya wazee wa
kale wa Mombasa (Mfunzi) ni kua watu hawa walikuwa wakipima mashamba kwa
vipande vya ngozi. Kasha jina hilo
likabadilika na kuitwa wavisai ama wakisai kwa kuwa walikuwa ni watu wakutoa
visa na mwisho ndiyo kuitwa Waswahili.
Lifwatalo ni shairi la kingozi limetungwa na Ustadh Ahmad Juma Bhalo
(Ustadh Bhalo)
Mwanzimle mlekele, ni mwina wa
bangu moyo
Moyo mtipi wa male, yasofupika
maziyo
Maziyo maku si mbale, maningayo
sifumbile
Siyo ndmi si nga soyo, maningayo
simbile
(Taa ya Umalenga u.k 22)
Licha ya Waswahili kuwa wenyeji
wa kitambo kuliko makabila mengine kwa mwenye kuelewa tarekhe (histria)
vizuri. Kinachosikitisha na kushangaza
ni kwamba kuwa lugha hii tukufu nay a kale ni ya kigeni, yaani asili yake si Afrika. Wanao shika kani (kulitiliya nguvu jambo) na
kulipigiya upatu suala hilo si rahisi kutamka fikra zao, kwa kucheleya
kuthibitisha kuwa ni wajinga wa histria ingawa Kiswahili kimethibitishwa kuwa
ni lugha asili ya kiafrika bila kusaza shaka yoyote.
Kuna
na wenye fikra ya kuwa utamaduni wa Kiswahili ni wa kigeni, na kupinga kuwepo
kwa watu waitwao waswahili kwa kusingizia kuwa maneno ya Kiswahili mangi
(mengi) yamefanana na kiarabu. Dai hilo
tukilipima vizuri tutaona halina mashiko maana takriban lugha zote ulimwenguni
zimeazimana maneno. Kwa mfano hebu tutizame kiingereza kilivyoazima maneno kutoka
lugha ya Kiarabu.
Na maneno yenyewe ni kama
yafwatayo;
1.
Amber (anbar)
2.
Crimson (Karmazi)
3.
Elixir (ikseer)
4.
Carat (Kirat)
5.
Cotton (al-Kutn)
6.
Sherbet (Sharabat)
7.
Tahini (tahina)
8.
Clipher /zero (sifr)
9.
Mask/mascra (mascara)
10.
Alcohol (al-kohool)
11.
Hazard (zahr)
12.
Caliber (kaleb)
13.
Jar (Ka’leb)
14.
Jar (jarra)
BASI KWANINI KIZUNGU KISIAMBIWE
NI KIARABU LAKINI KISWAHILI KUWA NI KIARABU??
Na ale wanaokubali kuwepo kwa
waswahili hutiya ila na kusema ati si kabila safi, na imetanganya (imechanganya)
yaani kuambiwa Kiswahili ni lugha ya kigeni hapa Afrika mashariki. Madai haya
yalizuka tu baada ya Africa kutawaliwa na waingereza, maana kabla ya ukoloni hapakuwako
na shaka yoyote juu ya kuwepo kwa waswahili, wala lugha yao wala utamaduni wao.
Tete hizi za tuhuma za waswahili
zilianza kuwashwa wakati wa ukoloni wa kiingereza, na zikabiririka zaidi pale
nchi za Afrika mashariki zilipokaribia kuwa huru. Kwa mfano wazungu walikuwa hawakubali kuwa
mwafrika ana ustaarabu au jambo lolote la kuweza kuonyesha ulimwengu umiliki wa
jambo Fulani. Ndipo leo tukaambiwa kuwa miji ya Kiswahili ni ya kiarabu kwa
ajili ya milango yaliotongwa (chongwa) kwa nakshi za kupendeza, mavazi, majumba
na kadhalika lakini ukiwauliza mambo haya yanatoka wapi sehemu za Arabuni
hakuna awezaye kukujibu.
Marejeo:
Shihabudin Chiragdin na Mathias
Mnyapala; Historia
ya Kiswahili.
Ahmad Nassir Juma Bhalo; Taa
ya Umalenga
Shihabudin Chiragdin; Kiswahili tokea ubantu hadi ki –
standard Swahili
John Ayto; Dictionary of foreign
words in English
Shihabudin Chiragdin; Kiswahili
na wenyewe
BY NAJEEB AHMAD NASSIR
JUMA BHALO
Cell No. 0729-906-761
E-mail nagibbhalo@yahoo.com
No comments:
Post a Comment