Uti wa Peremendi |
Uti wa peremendi ni uti ulotiwa maridadi au mapambo ya
karatasi za ragi ragi au zakungara na kupachikwa peremendi.
Uti huu hutengezewa
watoto siku za mfungo au mandari hasa mandari ya kukaribishwa mwezi mtukufu wa
Ramadhani. Maalumu siku ya kukaribisha
mwezi wa Ramadhani.
Watu huenda kuangalia mwezi kwa shime na vigelegele na
watoto wao waki chukua nyuti za peremendi.
Kujipumbaza kwa kula peremendi moja moja na kurukaruka kwa furaha na nyuti zao. Wakiimba kasinda za
kukurubisha mwezi Mtukufu wa Ramadhani kasida ( nyimbo) kama:
Children carrying Uti wa Peremendi |
Marahaba ya sharu Ramadhani *2
Maraba ya sharu saada waibada* 2
Prepared by:
Khadija Issa Twahir
Librarian
Lamu Fort Musuems.
very educative and informative. thanks
ReplyDelete