Tuesday, 7 May 2013

Uvuvi na Uhifadhi wa Papa....



Ismail Abdalla Shee
Papa ni samaki mkubwa katika bahari. Makao ya papa ni katika maji makubwa ya bahari hindi. Papa ni samaki wa maji ya chumvi na kwa hivyo hupatikana tu katika bahari ya hindi.
Chakula cha papa ni samaki wadogo na majani fulani ndani ya bahari.  Papa huvuliwa kwa kutumia Ndoana na Nyavu (Net). Uvuaji wa papa si kazi rahisi kwani ni mnyama mkubwa sana anayehitaji uangalifu na busara. Papa husababisha hasara kubwa kwa kukata vyombo vya uvuaji, basi huwa twatumia ujuzi wa kutega.



WAKATI WA UVUVI:
Papa huvuliwa wakati kuna giza  (Mwezi umeingia gizani) Nyavu huteremshwa ndani ya maji na kutega kabisa.

Papa akiingia kwenye mtego hushikwa na Nyavu; Kwa kweli papa hujitetea lakini mara mingi hafui dafu.   

Asubuhi na mapema wavuvi huteremka chini ya bahari kutazama kama wamefaulu kumshika papa . 


KUHIFADHI PAPA:
Punde tu papa akisha vuliwa, hupasuliwa  kisha hutolewa matumbo. Kisha husafishwa kutoa maji machafu na damu. Baada ya hapo hutiwa chumvi kukolea kisawa sawa kwa mda wa siku tatu.  Baada ya siku tatu, papa husafishwa tena kwenye maji ya Bahari mpaka kutoka chumvi yote iliyokuwa imetiwa awali.

Papa hukaushwa Baharini kwa wiki mmoja kwa jua ama upepo. Baada ya wiki papa hua ashakauka vizuri na wavuvi hutafuta soko na kuuza kwa jumula kwa wauzaji wa reja reja.

Papa huifadhika bila ya kuaribika kwa miaka miwili ama zaidi bora tu kusafishwa vizuri, chumvi ikolee vizuri na baadaye kusafisha tena kwa makini kutoa chumvi yote na kisha kukausha vizuri.

PAPA NI RASILI MALI YA WAVUVI:
Papa ni rasili mali ya wavuvi na pia ni kitoweo kinachotumika sana katika Pwani.   Papa ana faida nyingi sana:

Tiba Asili:
       Pezi (Fin) : Ni tiba ya kiwili wili  cha mwanamke na mwanamume, huongeza nguvu maradufu  asili mia mmoja.
        Liver Oil:  Hutibu cancer na T.B.
       Ngozi ya Papa: Hutengenezewa Viatu na mabegi haswa nchi za kigeni zilizoendelea. Hapa kwetu Kenya hatuja fikia kiwango hicho, kwani kunahitajika fedha za kutosha, vifaa na elimu
        Meno ya Papa: Huchemshwa, kasha kutolewa nyama yote,  kusafishwa na kukaushwa vizuri na baadaye kuuziwa watalii kama marembo ya nyumba 



Vyombo vya kuvua huwa vina pandishwa juu baharini kufanyiwa marekebisho mwezi unapo nga’ra, kwani wakati huo papa hapatikani.

Sufi
 









STORY BY
Masoud Rashid  na Ismail Abdallah Shee

FACILITATED BY
Fatma Mansoor

No comments:

Post a Comment