Friday 2 November 2012

Punda...

Salim Abdulrahim  Abdalla (Kidalla). 

Punda ni mnyama kama wanyama wengine walivyo umbwa, na hana tofauti yake kama wanyama wengine, kasoro na uzuri pia. Kwa hakika wanyama wote waliumbwa kwa wakati tofauti  na Mungu,  lengo la wanyama wote kuumbwa na Mungu ni kwa maslahi au matumizi au kutwi amri za mwanaadamu mfano:
Mnyama mkali Simba, ni mnyama mkali na adui mpaka kuitwa mfalme wa wanyama lakini anapokutana na mwanaadamu  kivilivyo anamtii na kuchukua amri zake.

Wanyama wote wa porini wanauasili, wanaaingiliana, mfano:- Ngombe/Nyati , Simba/Paka/Chui/Cheeta



Familia ya Punda ni wane wakiwa:
v  Farasi
v  Punda
v  Punda mlia
v  Nyumbu/Kiongwe
Farasi na Punda wazaa – Nyumbu (Mule)
Punda mlia na Punda wazaa – punda albino (stripe but different)
Katika wanyama wote hawa watembeleana (matting) hawana uadui, wanajihisi ni familia mmoja.

METHOLOGY YA PUNDA
ALIVYO UMBWA PUNDA (WAKATI)
Punda ni mnyama yuko tangu nyakati za mitume mfano: Punda ilitumika wakati wa mtume Nabii Nuhu  akijenga (safina) punda wametumiwa kwa usafiri na kubebea vitu tofauti, tofauti katika usafiri haswa kueneza/Kutangaza ujumbe wa Mwenyezi Mungu Mfano:

v  Nabii Issa (Yesu) – na wengineo walimtumia Punda sana kwa kazi yao ya Mungu. Imo katika Bibilia na Qur’aan kuhusu matumizi ya Punda ambavyo ni kama :
                                 i.            Pambo
                               ii.            Kipando
                              iii.            Katika mchezo.

(QUOTE FROM THE HOLY QUR’AAN)
ARABIC                                                                 KISWAHILI TRANSLATION
“WALKHAILA”                                                  FARASI
“WALBIGHALAH”                                            NYUMBU
“WALHAMIRA”                                                                PUNDA
“LITARKHABUHA”                                           MNAWAPANDA – WANYAMA HAO
« WAZINATAH »                                              NA MNAFANYA PAMBO, UREMBO
« WAYAHMILU »                                             WANAWABEBEA
« ATHKALAKUM »                                           MZIGO YETU
« ILABALADHIN »                                             PUNDA YUA TUBEBEA MZIGO WETU MPAKA KWENYE MJI YA MBALI
« LAMTAKUNU »                                             AMBAYO NI SHIDA
« BALIGHIHIILA BISHIQUIL AMFUS »      MZIGO MKUBWA KUIBEBA NA SAFARI YA MBALI

(The narrator here try to quote from the Holy Qur’an to show that the animals has been in existence since and during the times of the prophets and that the animals according the holy book are here to help us, to beautify our nature and environment and that should respect and follow orders from human beings. )

MATUMIZI YA PUNDA KWA MDA WETU WA LEO.
a.      Ubebaji wa mzigo vijijini khaswa katika umma wa kimaskini
b.      Kuguruta mkokoteni/Msukumeni
c.       Kubebea maji kutoka Mtoni/Ziwani/Visimani (haswa katika mji wa lamu na visiwani punda ina usaidizi mkubwa kwa wenyeji kwani mashamba ni mbali mno, kuteka maji pia ni kipande an vile vile ndio njia yapeke ya  usafirishaji, na ubebaji mzigo.
2. Kulima:
a.      Punda anatumiwa kuguruta gari/mkokoteni maalum kwamina jili ya kulimia ardhi
3.            Baadhi ya wanaadamu (Binaadam) wanamtumia kama chakula (kitoweo)
4.            na pia kuna itikadi ya kutumia cho cha punda katika kutibu maradhi ya watoto “kwa kufukiza moshi ya cho cha punda. “kwa sababu ya pepo mbaya au baba watoto ndege Ow
5.            mchezo ya mashindano ya mbio za punda khaswa katika wakati za sherehe kama (Swahili culture, Madaraka day, Mashuja day huwa ina fanna sana na kila mmoja hufurahia.
6.            Kwa kuwa sehemu za Lamu hamna usafiri wa gari (Kisiwani) punda wanatumiwa sana katika hali za dharura. Kubebeshwa wagonjwa wasiojiweza, ama mahtuti, mama mja mzito (nk) kuwasafirisha hospitalini kwa uduma za dharura (Yatumiwa kama Ambulance)

PUNDA: STORY BY
SALIM ABDULRAHIM ABDALLAH (KIDALLA)
PROFFESSION: MWALIMU
BAJUNI FROM LAMU
52 YEARS.

No comments:

Post a Comment