Saturday 1 September 2012

Ramadhan Fasting...


FASTING DURING THE MONTH OF RAMADHAN
The 5 pillars of Islamic faith

SAWM
Mohammed
Every fear in the month of Ramadan, all Muslims fast from dawn until at sun down. Abstinence from food, drinks and sexual relations with their spouse. The elder or on journey and menstruating, pregnant or nursing women are permitted to break the fast and make an equal number of days later in the year when healthy. Children begin to fast and observe prayers from puberty, although they may start earlier. Although fasting is beneficial to health; it is mainly a method of self purification. By cutting one from woundly comforts, even for a short time fasting person focuses on his or her purpose in life by constantly being aware of the presence of God. God states in the quran:”O you who believe! Fasting is prescribed for you as it was presented to those before you that you may learn from self-restraint. “Quran 2:183

MAPISHI USWAHILINI.

MAPISHI USWAHILINI KATIKA SIKU YA IDDI
MAANDALIZI

Maankuli ya siku kuu huandaliwa siku ya mwisho ya ramadhan. Vyakula hivi haswa ni vyakula visivyo vunda na huweza kutoharibika kwa muda wa wiki. Upishi huu huwa ni wa ustadi na taaluma ya uswahilini na kiarabu.vyakula zaidi ya aina tatu huandawa na akina mama. Ni jukumu la kiongozi wa nyumba ambaye haswa ni baba kuhakikisha maakuli ya siku ya iddi yako tayari.






AINA YA VYAKULA VYA IDDI
Mkate wa sinia
Mkate wa tambi.
Mkate wa mayai
Kokoto
Sambusa
Bokoboko
Halua
Vishete
Donasi

AINA YA MASHARUBETI
Kahawa chungu
Chai ya maziwa
Milk shake
Vinywaji vya matunda
Vyakula hivi ni vya kushilikiza tumbo, kwa kingereza huitwa”bites”, kwa maana haipaswi mtu ale mpaka ashibe. Kwa hivyo ale kwa uchache tu. Mapishi ya vyakula hivi ya kiwa tayari, huandawa mezani. Vyakula huandaliwa mezani pindi wanaume wakiwa msikitini katika swala ya iddi. Baada ya swala ya iddi, vyakula huwa tayari vimetapaka mezani. Wanaume na watoto huingia majumbani katika matembezi ya aila zao. Katika matembezi haya ndipo hukaribishwa mgeni kwa vyakula hivi.

MAPISHI USWAHILINI KATIKA SIKU ZA RAMADHAN
Maankuli katika siku za  ramadhan huwa vimegawanyika katika sehemu tatu. Sehemu hizi ni:
  1. Chakula cha kufungulia mwadhini
  2. Chakula cha futari
  3. Chakula cha daku
  4.  
CHAKULA CHA KUFUNGULIA MWADHINI
Upishi wa vyakula hivi huwa ni wa kwanza kabla ya vyakula vingine kupikwa.Vyakula hivi huwa havipikwi kwa wingi lakini hupikwa kwa uchache wa idadi ya watu pale nyumbani.Vyakula hivi ni kama:
v  Viazi vya kukaanga
v  Bajia
v  Kaimati
v  Katlesi na kababu.
v  Vinywaji pia ni muhimu kupatikana haswa  vinywaji vya matunda

Katika majumba mengine vyakula hivi hupikwa kwa wingi na hupelekwa msikitini kwa wale walio msikitini kufungua mwadhini hapo.

CHAKULA CHA FUTARI.
Upishi huu ni wa pili. Chakula hiki hupikwa kwa wingi kwa kutosheleza watu wote mle nyumbani na mgeni yeyote atakae kuja. Vyakula hivi huenda vikagawanyika katika mafungu mawili.Nayo ni:

CHAKULA KITAMU.
Katika futari chakula hiki huliwa mwanzo .Vyakula hivi huwa vinapikwa kutumia sukari nyingi hadi kuleta ule utamu wa chakula chenyewe.mifano ya vyakula hivi ni:
*      Viazi vitamu.
*      Tambi za mapapai.
*      Matangu.
*      Matobosha.
*      Vibibi.
*      Mabatali
*      Ndizi za kiume
*      Makoranya ya sukari.
*      Pojo.

CHAKULA CHA CHUMVI
Katika futari, chakula hiki huliwa mwisho.vyakula hivi hupikwa kwa kutumia chumvi katika upishi wake.Mifano ya vya kula hivi ni:
  • Mihogo ya nazi.
  • Chapati
  • Viazi vya nazi
  • Mkate wa fushi
  • Mkate wa mofa kwa nyama.
  • Viazi vya rojo.

Kabla ya kula vyakula hivi waswahili hunywa kinywaji maaruf kinachoitwa”shurba”. Kinywaji hiki ni cha uji wa ngano, mtele, nyama na bizari ya pilau. Mwisho wa kula vyakula hivi,waswahili hula/hunywa podini,kastadi au fahida.

CHAKULA CHA DAKU
Chakula hiki ni cha mwisho kuandaliwa baada ya vyakula vyote kuandawa. Vyakula hivi haswa ni vya carbohydrates na protini. Waswahili hula wali na mchuzi wa viazi kama daku lao. Daku huliwa saa tisa hadi saa kumi za usiku. Baada ya saa kumi ndipo saumu inapo anza na si ruhusa kwa mwislamu yeyote kula chakula chochote.

BEMBE
Chakula hiki huliwa katika saa tano au sita kabla ya watu kulala.Vyakula hivi haswa ni vya nyama.kwa mfano:supu ya nyama ama nyama ya kuchomwa na chipsi


No comments:

Post a Comment