'Elimu Asilia' is the Swahili equivalent for indigenous knowledge (IK). It acts as a common platform where National Museums of Kenya (NMK) libraries working with NMK researchers and volunteers interact with local communities and children in the collection, preparation, preservation, sharing, exchange and dissemination of IK on culture, environment, health and history for the memory of our nation for sustainability and eco-social development. For more, please visit http://www.elimuasilia.org.
Wednesday, 14 May 2014
Monday, 5 May 2014
NGOMA ZA KIPOKOMO
MAJ.
RTD SWALEH ODHA
CELLPHONE
NO:
0721 308 594
Email: odhaswaleh@yahoo.com
P.o. Box 87440-080100
Kiembeni Estate – Mombasa
UTANGULIZI:
alipozaliwa. Na pindi ukizaliwa Mpokomo huna tena hiari ya
kuchagua eti ugeuke na uwe Mkamba. Upende au usipende huna budi, utabaki kula,
kuvaa, kufurahi, na kuhuzunika.
NYIMBO
BILA NGOMA:
Mpokomo pia yuko na mila zake. Aliimba na kucheza. Aliimba
nyimbo za furaha na za huzuni pia, kwa sababu nyingi tofauti tofauti. Kwa
mfano, Mpokomo aliiimba Gassa/Kittoko
bila ya ala yoyote ile ya muziki, Aliimba bila ya kucheza na akiwa chini kitako
au kalala chali, hakusimama wima. Alikiimba kittoko
hicho aidha kutahadharisha kwa mfano (Jihadharini-Mende), Kejeli kwa mfano
(Ningali Kijana-Mende), Mapenzi kwa mfano (Together- Dr. Niko)na Hamasa kwa
mfano (Wanawake wa Ndera- Ise Viera). Nyimbo za aina hii huimbwa wakati wowote
hasa usiku. Na washiriki ni waume akiwepo mwana dada fulani pengine bibi wa
mmoja kati ya waimbaji tena mraibu wa nyimbo kama hizo. Hapa ni furaha tupu.
Kwani nyingi wa nyimbo hizo ni tumbuizo sana mume kumuimba mwanamke akimsifu,
akimsibu na kmuumbua watu wasikie urembo au ila yake muumbuliwa huyo pasina
mwenyewe kuwepo.
Kkosa
ya Dani ni mchezo wa watoto wa kipokomo ambapo ngoma haikutumika.
Michezo mingine ni watoto wa kike mingine ya kiume na mingine iliwajumuisha
wote. Mfano :
Majjilingao-Mchezo
wa watoto wanaposhikana makundi mawili wakipishana, wanapita kwa watoto wawili
walioshikana mikono wakiweka mtego wa kunasia
huku wanaimba usiku; -Haijjafiiko? He! He! e! -Majjilingao
ho ho lingo, majjilingao kittattafule.
-Ngao ya mabombwe, fumo
ddyakuttora.
Mpesi-Mchezo
wa watoto wanapoketi chini na kufanya dori, miguuni pana kitambaa kinazungushwa
huku na huko kushoto kulia na nguo imefunika gubi gubi mwanzo wa kiuno
kukiimbwa usiku; -Mpesie,
mpesi karitto, ikiya wenye bbabbaa.
Kode-Mchezo
wa watoto wa kike wakichimba kishimo ardhini na kuweka mawe. Hurusha moja juu
huku wakitoa na kusukuma zingine ndani kulingana na hesabu ya anayecheza bila
ya kuimba.Mchezo ni wa mchana.
Tteba-Mchezo
wa watoto hasa wa kike wakichora miraba ardhini kiasi cha wachezaji. Kipande
cha mawe hutupwa kinyumenyume na kikiangukia chini ni,’tteba’, mchezo huanza
kwa kurukaruka kutumia mguu mmoja mchana.
Pofu-Pafle-Mchezo
wa watoto wakifukuzana majini aidha mtoni au ziwani. Ni wimbo alafu mbio
wakipiga mbizi,mbio na kachombe kwa wimbo na kushangilia hasa nyakati za
mchana; -Pofuo-Pafle, Ddya mama- Ee, Aniaggiye-Ee,Ddyakwe!
Kinu
Kya Hawito-Mchezo wa watoto nyakati za usiku
wanapojilaza kwa amri ya mmoja wao, Ngalingaliee!;
Wanalala macho juu, wakinyoosha mwili mzima:
- Kinuo kinu kya Hawito,kya mchelechele
bbwoya bbwoya. –Mwezie-ee! Ee!,mwana chingicha mwana e mwana chingicha. -Chiko chikoo! Haya.
Fiche
(Rare)- Mchezo
wa watoto kufumba mkono nyuma migongoni na kuwambia wenzi wao watambue
walichoficha kuwa kikulia au kushoto.
Chio-Mchezo
wa watoto usiku wakifukuzana kwa zamu huku mmoja kafungwa kitambaa cha macho
asione na kwa nyimbo;- Amfu kattuttu-
ttuttuya, Nije ne fumo nije ne ttora? Njo ne fumo. - Chio kafwe macho, chio
kaona.Huyo mhangaisheni huyo.
Msupepe-Mchezo
wa watoto wa kupesapesa miguu hasa wanawake wakichuchumaa wawili wawili huku
wamegeukiana wakiimba na kupigapiga mchanga kwa mikono yao yote; -
Msupepe mchanga moto kwauona.
Kinamddabbe-Mchezo
wa watoto wakikimbizana ndani ya maji, nje na kwenye nyumba inayojengwa, hasa
nyumba ya miti miti.Mmoja anafuata mwingine amguse huku wakiimba;
- Kinamddabbe, unakyo-anakyo.Mbio…..!
- Kinamddabbe, unakyo-anakyo.Mbio…..!
Akosee-
Mchezo
wa watoto mchana kwenye dori hasa wanawake. Wanapokezana viguguta wakiimba;- Akosee nyaa zipho hamkuna mongo wa nyama. - Hoo hohoo Maramba kachi mwayano maramba. - Mamo niphe yukombe nikadye
marikka nyamo. - Kkosao mfunyeni kakosa.
Tandaule-Mchezo
wa watoto wakinyoosha miguu wakikaguliwa kwa nyimbo;-
-Mosia tandaule nyota kwa mlima katiti simbanyo naiya kwa ngombe bburanyinga ho!.Ngombe zenu bburungale kwa jili kwa ngombe. Mwananimbwa bbwa, maddindye ho, mwananimbwa bbwa!
-Moja na moja tandaule kwa magguyu ggwanya ggwanya, madindye hoo mwana nimbwa bbwa bbwa bbwa!
-Koko kokoya na malugga sangarse mumina. Mumino washindi shindi kajja waddoddo rubbesa. Abbo, kalimaddo, manguddo, ttalabba.
-Bbocha karara, magguyu chingicha, maneno mabaya, ttumbaku na nusu, nusura fwe!
-Dangulo dangulo, he ntanta yuwa, he yuwa yuwa mai, he mai mai kulotta, he kulotta kulotta simba, he simba simbaegguru, he gguru gguru kongwe, whende kwa vironda.
-Mosia tandaule nyota kwa mlima katiti simbanyo naiya kwa ngombe bburanyinga ho!.Ngombe zenu bburungale kwa jili kwa ngombe. Mwananimbwa bbwa, maddindye ho, mwananimbwa bbwa!
-Moja na moja tandaule kwa magguyu ggwanya ggwanya, madindye hoo mwana nimbwa bbwa bbwa bbwa!
-Koko kokoya na malugga sangarse mumina. Mumino washindi shindi kajja waddoddo rubbesa. Abbo, kalimaddo, manguddo, ttalabba.
-Bbocha karara, magguyu chingicha, maneno mabaya, ttumbaku na nusu, nusura fwe!
-Dangulo dangulo, he ntanta yuwa, he yuwa yuwa mai, he mai mai kulotta, he kulotta kulotta simba, he simba simbaegguru, he gguru gguru kongwe, whende kwa vironda.
Kwa
nyingi nyingi- Watoto bado wakiwa kitako na miguu yao
wameinyosha. Mwenye kuhisabu na aliye kiongozi anapitisha mkono na kuitingisha
kofia ya goti.
- Kwa nyingi nyingi kwa nyingi nyingi,kona unazimbika seggera unga, kuko kumbika kumbuka kwa nyingi nyingi. - Nkuruttume nyade, saanga nyade. - Ggumbu ggumbu ggumbu sole!
- Kwa nyingi nyingi kwa nyingi nyingi,kona unazimbika seggera unga, kuko kumbika kumbuka kwa nyingi nyingi. - Nkuruttume nyade, saanga nyade. - Ggumbu ggumbu ggumbu sole!
Dangalola-Huu
ni mchezo kama kinamddabbe, watoto hufukuzana kwenye uwanja bila ya kwenda
mbali. -Daanga loola-Samakia. Daanga
loola- Samakia. Hasina nampata- kwampata. Hasina nampata-kwampata.
Addirise
kiguyu-Mchezo wa watoto usiku wakishikana kwa pamoja na kurukaruka
kwa mguu mmoja huku wakiimba;- Addirise
kigguyuo e nangere, addirise kigguyu ajjeanisehe nangere. - Mwanahajjuyu ggoneyea keso maggura
haonana.
Mwaraggidde-
Mchezo wa watoto wakiwa chini kitako. Makundi mawili wamefuatana kwa mlolongo
na kiongozi wao akimlenga kwa bunda la nguo amchukue kila anayempiga.Wengine
wakijificha nyuma ya mgongo, huku wanaimba; -
Mwaraggidde- buu, mare hekaani-hekaani
Piropiro-Mchezo
wa watoto: -Piropiro chamara, asiduna nayawe.
-Ggoromicho ee! Micho, koonde na konde
Kwangure
mongo- Mchezo wa karibu kumalizia michezo wakati wa usiku watoto
wanasinzia ishara ya, ‘twende tukalale.’ Mistari ni miwili na kila kalabba watu
wawili hutawanyika na kutoka mistari yao upande upande na kwenda kwao;
- Kwangure mongo, haya. Mwanangu kalabba kalabba, haya.
- Mwanahajjuyu ggoneyea keso maggura haonana.
- Kwangure mongo, haya. Mwanangu kalabba kalabba, haya.
- Mwanahajjuyu ggoneyea keso maggura haonana.
Ngware
ni
nyimbo za Kipokomo za dini kwa ndugu wakristo hasa wa chini- (Milanchini) Tana
Delta. Huimbwa pia bila ya ngoma. Na sana, ni katika kusherehekea siku kuu ya
Krismasi na mwaka mpya. Huimbwa usiku wa kuamkia tarehe moja Januari na
washiriki ni wake kwa waume. Mfano wa nyimbo ni (Nilekeze Pwani) na
(Naikurubia).
Mattalili huimbwa bila ya ngoma na ndugu
waislamu wakati wa kuomboleza mtu akiaga na kabla ya kuzikwa. Wanawake
huizunguka maiti ikiwa kitandani na hata wakiwa nje ya nyumba huku wakilia.
Pindi mtu akifa iwe usiku hadi mchana mpaka azikwe, basi ni nyimbo tu za huzuni.
Himatta ni
nyimbo mashambani wanawake au waume wanapokutana kwa kulimiana. Ni jembe
nyimbo. Mfano (Kirura Ami Saduna Kirura).
Funya ni
nyimbo isiyo na ngoma kwa akina mama wapokomo. Mtu akiasi au kuwakosea
wanawake, aidha sheria zao kuvunjwa hasa na waume, wanawake hujumuika kwa
kumlipiza kisasi kwa kumkwangura kwa makucha au koa za mtoni. Humwimbia nyimbo
za kumuapiza na kumlaani huku wakilia kwa mfano (Whendeni wake whendeni) na (Kahuddawia).
Yavia ni hali
ya kumtoa kipusa na kumkubali katika hali ya umama. Kwamba sasa ametosha kulea
mume na nyumba yenye watoto. Kwamba akubali pia kujihusisha na hali ya maisha
kwamba aliyekuoa amekuchongea. Nyimbo zake ni;( Unauke kauyawa kafungwa polwe
ddya kichwa).
Sosobha ni
kibembeleza mwana. Mtoto anapolia aidha kulia kwa kumkosa mama mzazi, kulilia
njaa au maumivu, mkubwa wake humbembeleza. Ni kutokana na nyimbo ya aina hii
ambapo nchi ya Kenya imejipatia wimbo wa taifa. Mfano wa nyimbo hizo ni:
Woi woi mwano, wanyoko waime, waime mupunga, mupunga nde
wako, nde wako we kuddya, we kuddya unyamaiye njayoo!!( Oi! Mtoto nyamaza, ili wazazi walime,
ili walime mpunga, wewe unapenda sana kula mpunga,ukila tu, huwa unatosheka).
Mwana nyamaya mwana nyamayo, nyoko kenda pwanie, sowe kenda
pwanie! Na kuninyea na kunikojeeo.(Wee
mtoto nyamaza, mamako alienda mtoni, babako alienda mtoni, wewe unanikunyia na
kunikojelea).
Mddondo mddondo, hayuno mwana kaiyaani njoo muuddye.
Mddondo ywangu kichwa na mukia.(Mdudu
mdudu tafadhali, huyu hapa mtoto analia fika umtafune. Mdudu muhibu mwenye
kichwa na mkia).
Bee mddondo be! Bee mddondo be! Akuddobbee ni naani, whende
hukawabbigge wantu wa makondeni mwezi uyawa ni naani? (Ee mdudu! Ee mdudu! Nani alokuchokoza, tuende tukawapige wantu wa
mashambani. Mbalamwezi ulitoka, ni nani?).
Akiiyoiyo humudoma mikomani, naye kanamba nicheze. Kajjende
mwana, kajjende mwana naye njwa kiiyoiyo. Woi woiyee! Nyamaya kimye. Siiye
mwano, siiye mwana nunu, nyamaya kimi. Nyamayo, nyamaya mwana bee! Nyamayo,
nyamaya mwana bee kisasuzi. Kisasuzi mwana jjongoyoyo bee! (Analia na tumemuokota kichakani, na
ananiambia nimuimbiye. Mtoto hanyamazi, na katu hatulii bado analia. Lo! Mungu
wangu. Mtoto anyamaze. Usililie tena, usilie mtoto mzuri. Nyamaza kimya.
Nyamaza kasha utulie tuli. Na ukitulia nitakufurahisha na nikupe kitu kizuri).
Hayudde nkimo, hayudde nkima, hayudde nkimaa mkoshoro
karebbani kyambo (Ndiye Yule tumbiri,
tumbiri mgiryama anasubiri chambo).
Nyalilo
ni
mchezo wa watoto. Koko ya embe ilitobolewa na kuwekwa kamba katikati.
Inazungushwa koko hiyo na pindi ikivutwa huleta kasi fulani na mlio tosha kuitwa mchezo.
Mpheru
ni
mchezo wa watoto wa kupiga pia ya mti. Mti huchongwa kiasi na hutegemea aina ya
mti. Kibati kilichofungwa na mti kwa kamba hutumika kama usukani wa kuendesha
pia hiyo. Kila kinapotandikwa huvuma na kuleta mlio. Watoto wawili au zaidi
huvigonganisha vizuu hivyo na kinachozunguka na kizito kilichochongwa kwa usawa
huviangusha vingine dhaifu.
Mphujju
ni mchezo karibu sawa na mpheru wa kuzungusha pia. Tofauti ni kwamba, mpheru ni
kigongo cha mti wowote, huchongwa. Mphujju, ni mmea au mti maalumu unaoitwa
m’mphujju. Mti huo huzaa matunda aina ya mapera nayo huitwa mphujju. Tunda hilo
likikauka mbegu zake humwagika tunda likitobolewa katikati. Ni kama mpira
uutoboe juu na chini sawa sawa. Kijiti huchukuwa nafasi ya matundu yale mawili.
Kwa kutumia kijiti kilichojikunja cha upongoo kutoka kwa mkindu, kamba hufungwa
na ikizungushwa kwa kijiti cha tunda hili na kuachiliwa, tunda hucheza ngoma
nzuri sana hadi mwisho hupumzika. Ni mchezaji airudie kazi hiyo tena na tena.
Ggao
au
saddyekka ni mchezo wa wazee wa kiume wakijitumbuiza barazani. Huu ni mchezo wa
bao na unachezwa katika jamii nyingi duniani. Hauna wimbo ispokuwa kufanyiana
mizaha kama vile kwenye karata, keramu
na drafu.
NYIMBO
NA NGOMA:
Ngwili ni
nyimbo za ngoma kwa wanawake wa kipokomo mwanamke akizaa. Ngoma hii ala yake ni
debe tupu lenye kuleta makelele ili anayezaa asisikike sauti akilia kwa maumivu
hasa, anafichwa mtu mume asiijue siri ya uzazi unaumpata mkewe. Sauti ya hamasa
na kushajiisha wanawake wakutane kwa haraka ya, Yee Wake! Kisha nyimbo mfululizo pamoja na msukumo wa anayezaa,
huku wakimpiga na kumchuna. E kavyayo, ee
kavyayo! Yaani, o! amejifungua. Huimbwa wakati wowote, usiku au mchana.
Beni huimbwa sana na wanawake wa
Kipokomo kwa ndugu wakristo. Ni ngozi iliyowambwa kwa pipa kubwa litoe mlio
mzito na watu warindime kama ilivyo ngoma hiyo.
Samai ni ngoma ya kidini iliyoibuka katika tamasha za kuadhimisha siku ya kuzaliwa mtume Muhammad. Ni gwaride la sarakasi katika kuendeleza maghani ya maulidi barzanji na maulidi ya Kiswahili. Siku hizi, Samai imemea miguu na kuwa Zamuni, yaani kwata. Kama kawaida vazi la kanzu na kofia huvaliwa na vijana wakijumuika kando na wasichana wenye buibui. Ala za muziki ni ttwari, kigoma na zumari. Kwakuwa Mpokomo mwingi ni muislamu na amepakana na Mswahili, dini imekuwa ni mila yake na tamaduni ya uislamu katika kuijenga elimu ya dini na dunia alitumia ushairi, midundo na mahadhi ya kiislamu. Bila ya shaka hatuna budi kuingiza mada hii katika kundi hili la ngoma hasa ikikumbukwa ya kwamba ttwari pia hutumia ngozi kama vile ngoma. Katika fani hii, hata kama si mwanzilishi, Mpokomo amebobea na kukubuhu ujuzi mwingi wa ngoma hii zaidi kuliko kabila yoyote Pwani.
Mtu huzaliwa na akawa mtu mkubwa. Akiwa njiani mtu hupitia
mambo kadha wa kadha kimaisha ili akubalike katika hadhi, tabaka na daraja
aliyonayo. Kwa mfano kijana hutahiriwa ili astiri uume wake huduma bora kwa
mkewe. Kijana anapotahiriwa hupitia
daraja tofauti tofauti kule jandoni. Tohara (Ntinye) ni wakati wanapofanyiwa
kitendo na ambapo ni mwanzo wa ngoma, alafu Tohara (Riggi) wakati kijana
ashatahiriwa na mwisho ni Tohara (Lwebbe) kijana yuko tayari. Zipo nyimbo na
ngoma zake hapa: (Yarhigha na Mbele), (Lele Mwobbe) na (Usikile
Ubbaratte). Miri ndiyo ngoma
inayochezwa mchana kutwa na usiku kucha. Hujumuika wake kwa waume ili
kuwangojea vijana watoke jandoni na kuelekea makwao. Njuga za kutengenezwa na miyaa huundwa na kuvaliwa miguuni kwa
waume. Nkanyiki, shanga, ngorosho na
kkone, huvaliwa maungoni, kiunonu na shingoni. Mikononi wameshikilia nchoncho huku wamevalia ttama vichwani
mwao.
Wanawake nao ni Vumba
vichwani mwao, vichida shingoni, Hida maungoni pamoja na shanga. Nyimbo
za mchezo wa Miri ni nyingi, bali
sana ni (Jjabha Kayulelo)
Gganga ni aina ya ngoma ya Kipokomo
ichezwayo na wazee wakienda kurogga, wakitoa
huduma ya matibabu kutoa
jinni (Kidumbwe)na kufurahikia. Kwa
mfano wanaimba: (Gganga mekuya). Hapa ni furaha na mchanganyiko wa huzuni kwa
wote. Gganga na Miri ni viungo tosha kwenye halmashauri ya serikali kuu ya
wazee wa Kipomomo zama zile, yaani Kijjo
na Waggangana. Washingo huchezwa na watu wa kawaida kufurahikia jambo au
tukio Fulani.Wanawake kwa waume wenye rika moja ndio washiriki. Usiku au mchana ndio ngoma hunoga. Mfano wa nyimbo yake ni: (Muharia Ywangu).
Kittoko ni mchezo pia huchezwa wake kwa
waume sana kwa kufurahikia hali Fulani wakati maalumu kama vile baada ya kazi,
mavuno na arusini. Nyimbo kama (Mattolibi walonioza).
Ngoma hizi zote hapo juu hutumia ala aina ya ngoma kubwa,
ikiandamwa na kijigoma kidogo na kijidebe kilichogongwa na vijiti. Pembe au koa
hupulizwa kuletwa shangwe na vigelegele.
Mwaribe huchezwa kwa ajili ya furaha vile vile usiku
au mchana. Ngoma aina ya sondo na pia pilingwa,
vumi na uttasha ugongwao na vijiti hutumika. Mfano wa nyimbo iimbwayo
wakati huo ni: (Mboya si ddya kuhenda).
Ttaireni
ni
ngoma ya mzuka au kutoa mapepo yaliyowakabili wagonjwa. Nyimbo aina hii ndizo
huimbwa: (Farasi Wangu Panda). Mgonjwa anaweza kuwa mke au mume. Utasha, Vumi na kijigoma ndizo hutumika.
Wanawake wakijifungua (Ngia Nyumbani), hukaa ndani ya nyumba
kwa siku thelathini na tisa bila ya kutoka nje. Siku ya arubaini ni sherehe ya
kutoka (Yawa Nyumbani). Mchezo huu ni wa wanawake, tena wale waliopata bahati
ya kuzaa hata kama mtu amezaa kisha mtoto akafa hajazaa tena. Mfano wa nyimbo
zao ni (Hida Kiwaluwalu). Kidundu (Kikaha) ndicho kinachotumika kama ala ya
kuchezea ngoma. Ngoma ya aina hii ambayo kwa jumla ni ngoma ya akina mama
pekee, huitwa (Mea Wake). Bali watu
wa jamii ya juu huita Kingika (Wantua dzuu) na Kuphanga (Milanchini).
AINA YA
NGOMA:
Wapokomo wako na ngoma nyingi nadhani kuliko kabila yeyote
nchini Kenya. Ngoma hizi nyingi ni za
kuwambwa na ngozi aidha ya mnyama mwitu kama nyati, kuro, swara au mnyama wa
kufugwa kama mbhzi na ng’ombe. Mti maalumu kulingana na itikadi huchongwa kwa
namna Fulani ili kukidhi haja ya mchezo ule. Wakati mwingine chuma hutumika endapo mti
ulikosekana kuchongwa kwani si kila mtu huchonga. Vipo vifaa vingine vingi
vinavyotumika kuunda ngoma. Vifaa vingine ni siri ya wazee wa Gassa. Hivi
ndivyo vifaa vingine: Ngoma mzuka, ngoma ttaireni, ngoma wggangana, mwaribe,
pilingwa, vumi, ttwari, beni, uttasha na kadhalika.
Story Prepared By
Fatma Mansoor
Elimu Asilia , 2014
Research Institute of Swahili Studies in Eastern Africa (RISSEA)
National Museums of Kenya
Subscribe to:
Posts (Atom)