UTANGULIZI
TAREHE FUPI YA MUANDISHI
Abud Salim Mbarak Bazmaleh, |
Mimi nilizaliwa kati
ya 1944 na 1945 katika mtaa wa Kwajiwa – Malindi. Katika khati ya kuzaliwa
imeandikwa tarehe 15th September 1946. Tarehe hii iiandikwa kwa
munasaba wa kuniwezesha mimi kutukuwa mtihani wa KAPE (Kenya Asian Primary
Examination). Kwa wakati ule ukiopita umri wa miaka 14 huendi shule ya upili,
kwa hivyo marehemu Babangu (Mungu amuweke Pema – Peponi) wakati akiandikisha
hati ya kuzaliwa 1953 yeye na msaada wa msajili wakati ule wakaamua hivyo.
Nilipata ajali ya
kuunguwa tumboni katika mwezi wa Ramadahni siku moja kabla ya Idd Al Fitri
baina ya 1948 na 1949. Mimi sifahamu na wazee pia walisahau hawakujuwa ni mwaka
gani. Daktari wakati ule alikuwa Dr. Rozenger, yeye alimshauri marehemu Babangu
kunipeleka hospitali ya Makadara Mombasa.
Sipitali ya Makadara ilikuweko ambako sasa ni jingo la Posta Kubwa
Mombasa, Salim Road, (sasa ni Digo Road)
Mombasa nilikaa Mwebe
wa Tanganyika na ni kishughulikiwa na marehemu mjomba wangu na shangazi yangu
(Mola awarehemu wote na kuwaweka mahali Pema peponi) Mwisho wa mwaka wa 1951
nilirudi Malindi na Jan. 1952 ni kaingia shule ya Sir Ali bin Salim, nikianzia
Qur’aan class.
Jan 1953 nikaanza
Std. 1 ni kaendelea vizuri hadi std 7
mwaka wa 1960 mwezi wa November, ni kachukuwa mtihani wa KAPE na Al- Hamdulilah
nikapasi kwa “Grade III”.
Jan 1961 nikaanza
shule ya upili ya Arab Secondary (sasa
Khamisi Secondary School) kama “Boarder” mwanafunzi wa kulala shule. March 1964
nikiwa form 4 nikaacha shule kwa sababu zisioepukika. Mwezi ule nikapata kazi
katika idara ya “Government Coast Agency” kitengo katika Ministry of works.
Mimi nilikuwa ni kicheza
wa mpira wa miguu, mkimbiaji wa 220yrd na 400yrd wakati ule (sasa ni 200mt na
400 mts) na Hokey.
Nilijiuzulu kutoka kazi
ya serekali mwaka wa 1970. Baada ya hapo nikafanya kazi tafauti tafauti zilio
nipeleka Bungoma, Kisumu, Mbale Uganda na nikamalizia Saud Arabia. Saud Arabia
nilienda mwaka wa 1980 mwezi wa 3 na nilifanya kazi kwa miaka 14.
Niliporudi Malindi
ni Kafunguwa offisi ya udalali na nikapata liseni ni kafanya kazi kwa miaka 3.
Baada ya kuja mipango ya sheria mpya nikakosa liseni kwa kiwango cha elimu walicho
hitaji.
Nikafanya kazi kama
“Part time Accountant” kwa matajiri Fulani kwa vile nilikuwa na Diploma ya
“Book keeping” wakati ule ni kajishughulisha na Kazi za kijamii kwa upande wa
serekali na Mashirika yahaki za binadamu. Nilikuwa Treasurer wa Malindi
Constituency Aids kwa miaka 10. Wakati
huo pia nilikuwa katika Education Board kwa miaka 10 na pia Barani Secondary
School Board of Governors kwa miaka kumi.
Nilikuwa secretary
wa SUPKEM na pia Monitor wa FIDA “Chama kinachosimamia na kutetea hakia za
wanawake na watoto” Nikatuzwa Special Category Human Rights Award 2006.
Hata hivi ninashughulika
na kazi za kijamii kama mzee wa mtaa wa Kwajiwa na Secretary wa Malindi Council
of Swahili Elders.
Hii ndio tarehe
yangu kwa ufupi sana kwani hapa sipo pahali pakuleta tarehee yangu bali
nilitaka alioandika kumbu kumbu hii ajulikane alikuwa ni mtu gani na waina
gani. Pengine unaweza kupata maelezo mengine kupitia Google “BAZMALEH” ambapo
ukifika katika jina langu unaweza kupata maelezo zaidi.
Unaweza kuwasiliana
nami kupitia
P. O. Box 152, 80200,
MALINDI, KENYA
Email – abubazmaleh@yahoo.com
Mobile No. +254 724 336 113.
P. O. Box 152, 80200,
MALINDI, KENYA
Email – abubazmaleh@yahoo.com
Mobile No. +254 724 336 113.
LUGHA NILIO CHAGUWA
Tangu nilipokuwa
shuleni nilikuwa nikipenda kuandika makala ya Kiswahili na takriban mabuki yangu
yote ya shule nilikuwa nikiandika ushairi katika karatasi ya mwisho ya daftari
langu. Jambo ambalo lilikuwa likinipa
shida ya kupata daftari jipya kutoka kwa mwalimu likimalizika.
Pia nimeandika
vitabu kadha ambazo sikufaulu kuchapisha za ushairi na hadithi za kutunga. Kwa
vile napenda kuandika Kiswahili kwa ajili ya kuituza ndio nikaamuwa kuwa hii kumbukumbu
niandike kwa lugha ya Kiswahili – lugha ninayo ipenda na hujinaki nayo na
kuienzi.
SHEREHE
Malindi ilikuwa si mji
mkubwa uliokuwa na wakaaji wengi wakati ule. Pengine kama elfu 50 hadi 75 watu
wenyewe walikuwa wa kijuwana. Sehemu nying ya mji wa Malindi ilikuwa ni matuka
ya nyasi na miti ya mibaraka kwa wingi katika sehemu nyingi pamoja na mikunazi,
wakaaji wengi walikuwa ni Warabu Wahindi, Waswahili na Wagunya (Wabajuni). Wamijikenda
walikuwa wakiishi nje ya Malindi isipokuwa idadi ndogo sana waliokuwa wakifanya
kazi ofisi za serekali au kwenginepo.
Sherehe nyingi hasa
za harusi huwa ni za mchanganyiko, sherehe hizi hushiriki wakaaji wote wa Malindi
hata huzuni, kukihudhuriwa na watu bila ya ubaguzi wowote.
Kwa sababu nimeweza
kuhudhuria sherehe nyingi naweza kuzieleza tarabitu zote, zilioko katika baadhi
ya ngoma ambazo nilioshiriki au kuona kama vile Gwaride Shabuwani na sherehe ya
Maulidi. Hapa chini mimi nitaeleza kwa kadri ya uwezo wa kukumbuka hizi ngoma
za kitamaduni ambazo mimi ninazi fahamu au nilishiriki
NGOMA ZA KITAMADUNI –MALINDI
Hapa nitajaribu
kuzieleza ngoma hizi za kitamaduni kwa uwezo wa ujuzi wangu na vile ninavyo
zifahamu. Ngoma zenyewe ni kama zifuatavyo 1. Gwaride 2. Shabuwani 3. Kirumbizi
4. Goma 5. Vugo 6. Lemama 7. Mwaribe 8 Gonda
na 9. Sherehe za Maulidi
1. GWARIDE
Gwaride Malindi kulikuwa na vikundi viwili kimoja kikiitwa
Kingi na cha pili kilitwa Sultan. Kikundi cha Kingi kilikuweko upande wa Kwajiwa
kuelekea barani na kikundi cha Sultani kilikuweko Shella.
Hata hivyo vikundi vyote vilikuwa, vimekusanya wafuasi
kutoka Kwajiwa, Shella Bomani na Barani. Kuna wafuasi pia walotoka Ganda, Mkaomoto,
Mgurureni, Mere na Kakuyuni wafuasi walikuwa ni wa mchanganyiko wa makabila
a)
Viongozi wa
kikundi cha Kingi walikuwa kama wafuatao
i.
Marehemu Uba –
(Abdurahaman A. Chocha – kama captain
ii.
Mzee Musa
marehemu
iii.
Marehemu mzee Khamisi
Dobi – mpigaji gwaride.
iv.
Marehemu – Mwakatwa
mpigaji tarumbeta
v.
Marehemu Pekele –
mpiga kigoma
b)
Viongozi wa
kikundi cha Sultan
i.
Marehemu Bakari Ali
Marehemu mzee Ali Shiheli – pia mfadhili
ii.
Mzee Omar Shee mpigaji Tarumbeta
Marehemu Duru mpiga tarumbeta
iii.
Mpigaji gwaride
marehemu Mbaruku / drama
iv.
Mpigaji gwaaride
marehemu Azizi Breki
c) Kwa kawaida Gwaride lilikuwa na vikosi vifuatavyo
c) Kwa kawaida Gwaride lilikuwa na vikosi vifuatavyo
i.
Kikosi cha wazee
kikogozwa na captain
ii.
Kikosi cha Arab
Scouts
iii.
Kikosi cha Navy
na Askari wengine.
iv.
Kikosi cha Cowboy
d) Mimi nilikuwa ni
mfuasi wa Kingi na nilicheza katika kikosi cha Arab scout, wakati huo nilikuwa
na umri kama 12 and 13 hivi.
i. Arab Scout
walikuwa wakivaa vazi la suruali nyeupe na shirt jeupe na kichwani kuvaa igal – igal ni kitambaa unachovaa kichwani na
huzuiliwa na mfano wa kamba nyeusi uliosukwa vizuri sana – igalinatoka Arabuni
na sana ni zawadi wanaokwenda Makka kuhiji huleta kama zawadi. Mchezo wa kikosi
cha Arab Scout ni mchezo ulio makini wenye utulivu na kuchezwa kufuatia mlio na
mdundo wa ngoma.
ii. Kikosi cha wazee
huwa kina ongozwa na captain ambae anakuwa mbele. Wazee huwa wamevaa rasmi nguo
tafauti tafauti za kupendeza. Wengine huwa wamevaa suti natai, wengine suruali
na shati na dhalika wote ukiwangalia wako maridadi kwa mapambo ya namna
namna.
iv. Pia ni mchezo wa makini wenye haiba ya kipekee na mara nyinge huenda march kama askari wa kweli.
v. Kikosi cha cowboy –kikosi hichi watu wana valia kama cowboy katika picha za Kiamerika, kiononi
ametia pastola ya bandia na kamba ya kufungia ngombe ame funga kiunoni – kama vile Waamerika wanaochunga ngombe huvaa na kuonekana katika film za cowboy za Kiamerika.
Pia huwa wamevaa
viatu venye visigino vya juu vikifunguwa hadi juu ya macho ya miguu. Kuchezwa kwake
nikwa vishindo na machachari, wakirusha kamba na kupiga firimbi. Mchezo wa
cowboy haukuwa ukichezwa kwa makini kabisa, ulikuwa na harahati nyingi za
kimazoezi kama mchezo wa P.E shuleni. Mchezo wake ulikuwa ukifurahisha sana
mara nyingi wao hawafuati mtindo wa ngoma inopigwa bali walikuwa na miondoko
yao wenyewe wakifuata kiongozi wao anavyo fanya.
e) Kawaida
upande wa Kingi walikuwa kuanzia Captain 1) Wazee 2) Navy, 3)Arab scout and 4) kumalizikia Cowboy. Wapigaji ngoma
na tarumbeta wali kuwa mwisho wa vikosi vyote.
f) Kingi
walikuwa wakianzia ngoma upande wa “Baipasi” sasa round about “ kufuatia njia
hii kuja chini hadi kwa hoteli ya Manos na Said Kafiri (wakati huo hapakuwa na
majengo ya hivi sasa kama Wananchi Bar, Lamu Hotel, Tana Hotel na Habib Bank,
mjengo mengi ni mapya.
Ngoma huanzia
saa kumi na moja na nusu au kumi na mbili hadi ififikia karibu na Wananchi Bar,
huwa ni takriban saa moja usiku. Kipande cha
Wananchi Bar mpaka Habib Bank kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu unusu usiku.
Hii huwa ni kapande cha kuchezwa ngoma ya Mserego kwa makini na utulivu sana.
Kila mchezaji alikuwa akicheza kwa madaha na kuonyesha ubora na uhodari wake
wakucheza. Huu ndio wakati watu wana kuja kuangalia wakiwa ni wengi sana.
Wengine huwa wana watazama marafiki zao, au wazazi kuwatuza watoto wao wanao
chezo. Wengine wali
kuwa – wakizawadiwa mashada ya kila aina ya usimini, viluwa, makoja ya karatasi
– tuseme kila ina ya mapambo huwa wakipambwa wachezaji, hata pesa.
g) Tukiangalia
upande wa Sultan ni dhamu yake hufanana sana na Kingi. Wao huwa wakianzia bara
bara ya kutokea kwa Bakshweni yaani Malindi Cylce Mart wakushukia chini kupitia
kitanguni kwa Masoud kuja Kitaru cha Naran na kupita kwa Abdalla ngozi (sasa
Dosajee) kuja kwa Bawali haluwa mpaka msikitiwa Bohora. Nidhamu za kucheza ni
zile zile kama za kingi bali kula kikosi na kikundi kinaonyesha uhodari na
ujuzi wake kuweza kuvutia watu wengi kuja kuwaangalia
h) Gwaride
huchezwa kwa musimu yaani katika miezi mitatu ya Kiangazi na ilikuwa ikichezwa
kila siku ya ijumaa pili jioni – kuanzia saa kumi na moja na nusu hadi saa tatu
na nusu usiku.
Kingi humaliza
dori lake kwa marehemu mzee Swaleh Chocha –baada kutoka kwa marehemu mzee Uba
kupiga saluti wana kuja kwa marehemu mzee Swaleh kupiga saluti na kuvunja ngoma
Upande wa
Sultani vile vile ili kuwa ikipitia kwa marehemu mzee Shikeli na marehemu
Bakari Ali na kumalizikia katika uwanja wa marehemu Abdalla Swaleh –Mkwajuni
i) Katika Gwaride
kuna mambo ya ziada nyakati za mwisho wa musimu kwani kila kikundi kinataka
kipate ushindi wa mwaka ule. Kila kikundi huleta wachezaji wa sarakasi kutoka
Mombasa na Tanzania wa kila aina, kama miguu ya miti, wenye hutowa moto
midomoni, kuna wenye vituko aina aina. Mimi nitaeleza siku ya mwisho (finali)
yani siku moja katika maisha ambayo ilinivutia na kunifanya kuto sahau ni siku
hii ya finali.
Kwa upande wa Kingi wao waliunda meli kubwa sana
iliwekwa juu ya lori, meli hii iliundwa kama manuwari ya kweli ambayo ilikuwa
na askari wa kawaida wa navy pamoja na maofisa ikienda taratibu juu ya lile
roli – katika udogo wangu mimi nilidhania ni kweli manawari ya kweli na wale
askari wa ‘navy’ ni wa kweli.(manwari ni meli ya kivita ya navy).
Yule captain alisimama ma kwenye Manwari (meli ya
Navy) na mkewe amevalia veli na taji kama malkia. Huku wakipungia mkono watu,
niilifikiri ni mfalme na malkia kweli vile walivyokuwa wamevaa, kweli ilikuwa
jambo la kupendeza na la ajabu sana.
Manwari ilikua imekuja saa za mwisho baada ya saa mbili
usiku lakini kabla ya hio manwari, kulikuwa na mtu aliekuwa akitembea juu ya
kamba akicheza na moto.
Zamani Malindi kulikuwa na minazi mingi ubavuni pa
hoteli ya Manoos palikuwa na mnazi na nyuma jumba hili sasa la Lamu Hotel kulikuwa
na mnazi mwengine, takriban masafa ya futi 150 au 200. Kamba ilifungwa kutoka
mnazi uliokuweko kwa Manoos hadi katika manzi uliokuwako juma ya Lamu hotel.
Yule mchezaji alipanda mnazi ulikuwako nyuma ya Lamu
Hotel ambao ulikuwa haunekani na watu. Tulishutukia tunaona mtu akitembea juu
ya kamba huku akirusha moto huku na huku mara ingine alitowa moto mdomoni. Watu
wote wakasahau gwaride wakashughulika kuangalia sarakasi hii. Alio kuwa
akiyafanya ni mambo ya ajabu sana. Mara nyingine kujifanya kama anataka
kuanguka, kisha akarudi kama alivyo kuwa, watu wakaona mambo ya ajabu ambayo
sote hatujapata kuona.
Nilielezwa kuwa Yule mchezaji wa kamba ameletwa kutoka
Tanganyika (Tanzania) na wengi walikuwa ni hisia kuwa moto ulikuwa ukitoka
mdomoni ni kweli bali ni kwa ajili ya
mafuta aliokuwa akitaia mdomoni na kuvuzia huku ameshika moto mbele ya mdomo
akaonekana kama unatoka mdomoni.
J) Kwa upande wa Sultani walikuwa na vioja vyao pia.
Walileta watu wa maguu ya miti wakiteza kila na
namna wakirusha vitu na kunyaka na kutowa moto midomoni.
Onyesho kubwa la ajabu ilikuwa kuba kubwa liloundewa
kwenye lori. Katika kuba kulikuwa na watu walicheza kama nachi za kihindi za kupendeza
na kuvutia sana kwa vile watu wengi wa Malindi nyakati hizo walikipenda sinema
za Kihindi.
Maonyesho haya ya kiajabu huja saa za mwisho ikiwa
kila kikundi kikivutia kwake. Hizi ndio sherehe za mwisho zenye kuonyesha upeo
wa uhodari wakucheza wakishindana kupata
jamhuri kubwa ili kupta ushindi wa mwaka ule.
k) Kawaida Gwaride huanzia saa kumi na mbili jioni kilile
cha mchezo ni kutoka saa mbili usiku hadi saa nne kuanzia saa nne huwa zinapandia
mitaani Kingi ina elekea Kwajiwa na Sultani huelekea Shella ikifika saa nne
unusu usiku huwa ngoma zamesha vunjwa na kila mtu ameenda kwake.
Nyimbo mashahuri sana zilikuwa zikiimbwa na zinao
hamasisha wachezaji wa gwaride kwa mfano.
Endao pwani na Nende
Nenda kwamwambie
Kenya basi haina ahadi
Haiati mzishiwe
Chicha na kanada
Shauri yao.
Ya pili – Nyumbu eeeerero nyumbu rero
Watetea mwana siwako
Watetea mwana siwako
Nyamaza Kingi kulia.
2.
SHABWANI
a)
Hii ni ngoma ya Kiarabu,
hasa kutoka jamii ya Kihadharami. Ilifika hapa Malindi na Mombasa karne nyingi
ziliopita na kutezwa katika sherehe nyingi kama za harusi na za Maulidi wakati
wa zefe. Shabwani ni ngoma ambayo inachezwa kwa harakati za kuruka ruka na mikononi
wenye kucheza huwana bakora au fimbo
wakati wakicheza zile fimbo huwa zikirushwa rushwa juu na huku wakiiimba.
Arabuni waliokuwa wanao cheza huwa wana tumia panga lakini hapa watu hutumia
fimbo au bakora.
b)
Ngoma ya shabwani
hutumia ngoma moja au mbili, matasa na vigoma. Ngoma ya tasa ni huambwa kwa
ngozi.(yaani karai liloombwa kwa ngozi)
c)
Hii goma ya tasa
ni lazima iwe itakanzwa moto wakati wa kutumika na kupigwa kwa vijiti viwii
vipana virefu. Kupata mlio mzuri ni lazima vile vijiti viwe vigumu na tasa limeoka
moto uzuri.
d)
Kuanza kucheza
shabwani – wachezaji hujipanga laini mbili za kulekeana yaani kuangalian uso
kwa uso. Wakati huo wenye kupiga tasa huwa wanazikanza moto.
e) Kiongozi huingia
katikatii na kuanza kutowa shairi la fumbo na kulekea laini moja. Na wale
wachezaji waliolekewa waitika kama vile kiongozi anavyo imba. Wakisha itikia
anazungukia laini ya pili kutowa shairi ya jawabu yahilo fumbo. Sasa wachezaji
wakaanza kuimba na kujibanza wakati huu wenye ngoma wataanza kupiga na shabwani
kuanza ana wachezaji wote wakielekea upande moja wakiruka ruka na kurusha fimbo
/ bakora walizo nazo mikononi mwao kwa nidhamu ya kufuatia mdundo wa ngoma.
f) Shabwani – watu
waenda wakicheza, wakifika mita 150 au 200 mita, hubidi wenye kucheza waanze upya,
kwani tasa huwa limeanza kupoa na mlio huwa si mzuri. Shabwani itaanzwa kama
vile ilivyoanza mwanzo.
g) Shabwani zilikuwa
ni tatu, kutoka Mombasa Malindi na Mambrui. Shabwani hizi mara nyingi hushindana
wakati wa sherehe za Maulidi.Mamburii na Malindi Shabwani ya Malindi na Mambarui
walikuwa wakishindana wakati wa sherehe za Maulidi ya Kipini.
h)
Shabwani ilikuwa
ikichezwa sana katika sherehe za harusi wakati wa kutia hina na kumnyowa bwana
harusi na kumpeleka nyumbani.
i)
Shabwaini
huchezwa siku ya kutiwa hina Bwana harusi. Sherehe kufanyika usiku wa siku ya
kuingia ndani, siku ya kuamkia nikaka. Sherehe hii hufanywa katika uwanja
karibu na nyumba ya bwana harusi nayo inaanza baada ya ishaa na kuendelea hadi
saa nne usiku au zaidi.
j) Katika sherehe ya
kunyolewa bwana harusi ambayo hufanyika katika
mmoja ya kitanguni(bustani ya miti ya matunda na maua) Malindi kulikuwa na
vitangi vitatu, kitanguini kwa marehemu Maalim Balala, kitanguni kwa kina
Marehemu Masudi (sasa kuna star Hospitali) na kitanguni cha Barani (sasa kuna
gareji ya marehemu Mohamed Mzuengu nyuma ya duka ya la Sheikh Salim).
Sherehe ya kunyolewa, bwana harusi akiwa ananyolewa shabuwani
wakati huo huwa inachezwa. Akisha kunyolewa huchukuliwa Yule bwana harusi na
shabwani hadi pale atakapo funga, Nikaha.
Akisha funga Nikaha baada ya ishaa, bwana harusi hupelekwa kwa mkewe
kutowa mkono na kisha kupelekwa kwake nyumbani.
k)
Shabwani ya
Malind ilikuwa ikisimamiwa na
(a)
Marehemu Swalehe
Chocha,
(b)
Marehemu Salim
Bazmale
Shabwani ya Mambrui ikisimamiwa na:-
(a)Marehemu Omar Alwan
(a)Marehemu Omar Alwan
(b)Marehemu Mzee Nassor
3. KIRUMBIZI
a)
Kirumbizi
huchezwa sana na Wabajuni na Waswahili lakini huchezwa katika sherehe zote za
harusi hata ya Kiarabu. Kirumbizi Kawaida huchezwa na wanaume pekee, watu
hufanya duwara kubwa wa chezaji na wano piga ngoma huwa ndani ya hilo duwara au
boma. Kirumbizi, ni mcheza wa bakora ua fimbo Watu wa kucheza kirumbizi katika
harusi. Wanawake huwa kwenye jukwaa lilositiriwa na uwa wa makuti. Wale wanawake
huwa wanawaona wanaocheza kirumbizi lakini wachezao na wanaume wengine hawaoni
wale wanawake. Wale wanawake husherekea nakushangilia kwa kupiga vugo na kwa
nyimbo.
b)
Kawaida ya
kirumbizi inategemea Yule mwenye kuitayarisha, kuna wanao cheza kwa siku moja,
siku tatu au siku saba. HIvi inatagemea mfuko wa Yule mwenye kutayarisha au
mwenye kuweka kirumbizi na kuandaa.
c)
Siku ya mwisho ya
kirumbizi, ni siku ambayo Bwana harusi huja uwanjani na yeye kushiriki.Hapo
huwa ndio kilele cha sherehe hio. Bwana harusi – yeye huwa amepambwa kwa
mashada, viluwa na makoja. Yeye huinuliwa na baba mkwe na kucheza nae. Kucheza
kwao huwa ni kwa taratibu na heshima pamoja na taadhima kubwa. Huko wanawake
wakishangilia zaidi ya siku zilio pita.
Wakati bwana harusi akicheza watu hugaiwia maji ya sharebati
na tambuu. Tambuu hizi ni tafauti kwa vile huwa zina pambwa kwa karafuu.
d)
Uchezaji wa
kirumbizi huchezwa kwa watu kutumia fimbo au Bakora, mchezaji huchukuwa fimbo
au bakora na kuingia uwanjani na kumrushia fimbo au bakora Yule atakae cheza
nae.
e)
Wakiisha ingia
kiwanjani huwa wanacheza kwa upole n atarabibu kwa kufuatao mdundo wa ngoma.
Wachezaji huzunguka wakicheza kwa mfano wa koo la tausi au bata mzinga anapo
mtaka tausi au bata mzinga jike. Huzunguka wakicheza kwa haiba na utaribu wenye
kupendeza sana. Ngoma ikitangwanya na kulia kwa sauti kubwa, sasa wachezaji
kurushiana fimbo au bakora moja moja. Wala hakuna kurushiana kwa nguvu za
kupita kiasa bali kwa nguvu ya wastani kwa haiba na madaha.
Yule aliorushiwa bakora au fimbo mara ya kwanza ataichukuwa
fimbo au bakora ya mwenzie amrushie mwengine na hivi mchezo uanandelea.
f)
Ngoma zinao tumika
ni ngoma za kawaida na msondo, tasa, zumari au tarumbeta.
4. GOMA
4. GOMA
Goma hii huchezwa sana
na Wabajuni. Ngoma yenyewe ni ngoma ambayo huchezwa bila vishindo wala harakati
nyingi. Ni ngoma inayochezwa kwa ustarabu na haiba ya juu.
Wachezaji hucheza kwa
makini wakifuatia mdundo wa ngoma. Huechezwa kwa makini sana ya hali ya juu ya
utilivu kutaka kuona harakati zao za kucheza ni lazima uwe na makini kutizama
ndio utaona harakati za kucheza.
Wachezaji huwa wamevaa
kanzu nyeupe na kofia za vito, bakora mkono wa kulia. Bakora huwa imewekwa
begani na huwa inainuliwa mara moja moja kufuatana na mdundo wa ngoma.
Wachezaji huwa wamepambwa kwa mashahada ya maua na pengine kosaja la pesa.
Wapigaji ngoma huwa
wanaelekea wale wachezaji. Ngoma zenyewe ni zile za kawaida kama a kirumbizi,
tasa na zumari. Goma inaweza kuchezwa
kwa muda mrefu na huku watu wengine wakiimba nyimbo tafauti tafauti.
5.
VUGO
Hii ni ngoma inayochezwa na wanawake wa Kibajuni na Wakiswahili.
Ngoma yenye hutumika katika sherehe nyingi kama nilivyo eleza hapa nyuma katika
kirumbizi na kupeleka bi harusi na shrehe nyinginezo.
Ngoma huchezwa na wanawake, wakiwa wameshika pembe na kigongo
kidogo cha kumpigia pembe. Pembe hupigwa kufuata mlio wa ngoma na mara moja moja
huuinuliwa juu kichwani zikipigwa kwa nguvu huku wakiemba mashairi mengi mazuri
Ngoma hii huchezwa na mchanganyiko wa wanawake lakini
zaidi ni Wabajuni na Waswahili.
6.
LELEMAMA
Hii pia ni ngoma ambayo Huchezwa na Wabajuni,
Waswahili na wazaliwa wa Kiarabu. Ngoma hii sana huchezwa siku za harusi. Pia
hii inategemea wezo wa mtu anae cheza au anaendaa harusi, yaani kucheza kwa siku
moja au tatu au zaidi lakini hazipitishi saba.
Ngoma yenyewe huchezwa na wanawake wanao vaa kanga
peikee. Kanga ndio nguo rasmi ya kucheza lelemama, kawaida lelemama huchezwa
ndani ya uwa yaani boma liljengwe kwa makuti wanaohudhuria ni wanawake pengine isopokuwa
wale wapigaji ngoma huwa waume.
Lelemama huchezwa na wanawake wakiwa juu ya mabao
wakiwa wamevalia leso zao (kanga) zilio safi na mara nyingi huvaa sare,
wachezaji huwa wamejipamba kwa vilua, mashada ya asmini yalio fungwa vichwani.
Kila mchezaji huwa ana vigongo viwii ambavyo urefu ni kama inchi 6.
Lemamama huchezwa kwa makini na kuyumba yumba kulia na
kushoto kwa kufuata mlio wa ngoma, lelemama pia huchezwa kwa makini na utulivu
wa hali ya juu. Wanawake wengine huwa wamekaa chini kwenye majamvi wakipiga makofi
na kuimba. Kufuata sauti ya zumari au tarumbeta.
Kulikuwa na vikundi viwili vya lelemama cha kwanza
Karisosa na cha pili ni Sultani Karisosa hilikuwa ni kikundi ambayo kime jihusisha
na wafuasi wa gwaride la Kingi na Sultani wamejihusisha na kundi cha Sultan.
Mara nyingi walikuwa wakishindana.
7.
MWARIBE
Mwaribe haswa ni ngoma ya Kiswahili lakini huchezwa na
makabila kadhaa. Kawaida huchezwa na wanaume na wanawake. Waume wakiwa upande
mmoja na wake wakiwa upande mwingine wakiwa wameangaliana uso kwa uso.
Ngoma zinaotumika ni za kwaida lakini hutumika na msondo
(msondo ni ngoma ndefu) mwenye kupiga huwa amesimama na ngoma ameitia katikati ya
miguu ikizuiliwa na magoti mawili. Pia hutumika na zumari.
Ngoma ikianza kuchezwa na watu hucheza na kuimba
mwanmke huja katikati akicheza kwa muda kisha akaenda upande wa wanaume akamtowa
mwanamume kucheza nae, watacheza pamoja kwa muda pale katikati. Kiasha yule mume
wa atamtowa mwamke mwengine naye watacheza pamoja kwa muda pale kati kisha yule
mke atamutowa mwamume mwingine na wataendelea kucheza yule mwanamke wa kwanza
atatoka katikati ya uwanja. Mwanamke wa pili atacheza kwa muda wa baadae
kumtowa mwanamume mwengine msitari wa waume na ngoma kunaendelea. Ngoma
itaeendelea hivi hadi kuvunjika.
8.
GONDA
Gonda ni ngoma ya Kimijikenda ambayo huchezwa sana na
Wagiriama. Ngoma hii kuchezwa kwa utulivu sana na ngoma yeyenye kuchezwa kwa
mdundo mzuri hasa kwa wanaume. Wanaume wanaocheza Gonda huvaa shuka ndefu yenye
maridadi ya matavuo chini ukingoni. Kifua huwa wazi lakini huwa kimepitishwa na
ukanda wa nguo iliofungwa kwa umeridadi kutoka bega hili kushuka katikati ya
mwili hushukia kiunoni upande mwengine yaani hutoka bega la kulia ikishuka upande
wa kiuno wa kushotoni, nguo zenyewe huwa zinatiwa maridadi mazuri. Pia ukanda mpana
ambao hufungwa kiunoni namna ya pekee. Kichwani wanavaa kofia za tarbushi
nyekundu.
Ngoma hii huchezwa sana na wazee ambao hucheza kwa
madaha na Makini huku wakirusha migwisho na kupiga firimbi gonda ni ngoma yenye
haiba sana na huchezwa sana na wazee katika sherehe maalumu.
Wanawake kama kawaida huwa wamevaa mahando yalio
malkubwa, huku wakicheza na kuimba na kupiga vigelegele.
Waume hucheza na wanawake wakiimba, huku waume
wakicheza miguuni huwa wamefunga njuga na mikononi wamevaa meridadi
ya ngozi. Wakicheza hutetemesha mikono na kupiga miguu yao chini ili zile njuga
zipate kulia.
Ngoma zake ni za kawaida na msondo na kupiga debe kwa
vifimbo pia huvuvia pembe na kupiga zumari Ngoma hii huchezwa hadi wenyewe
kuchoka. Gonda ni ngoma ninaopenda nawe utapenda kuangalia sana.
9.
MAULIDI
Maulidi singoma bali ni sherehe ya Kiisilamu ya
kukumbukwa kuzaliwa kwa mtume Mohamed (S.A.W) Maulidi huwa yanasomwa wala
hayachezwi.
Kuna misikiti mengine husoma maulidi kila siku ya
alkhamisi baada ya swala ya magharibi. Pia husoma katika sherehe za Nikaha
yaani harusi au mtu akipenda kusoma maulidi.
Maulidi inatoka katika neno la Kiarabu “Maaulid”
kuzaliwa yaani “Birthday”
Sherehe kubwa ya maulid husomwa mara moja kwa mwaka katika
mwezi wa mfugo sita Kiswahili “Rabi – Awal” karibu, sherehe hii ya maulidi husoma
katika miji kadhaa kama vile Lamu, Mambrui, Kipini, Malindi, Mombasa na
Nairobi, na kwenginepo
Siku ya maulidi katika miji huanzwa kwa sherehe za Dhefe,
dhefe ni sherehe moja huchezwa na watoto na wazee kila madrasa ambyo
inayoshriki ina dhefe yake. Kila dhefe, inakasida maalumu wanazo ziimba za
kusifu mtume Mohammad (S.A.W)
Kuna kwasida za Kiswahili, kiarabu na siku hizi za
kimijikenda.
Dhefe huanza baada ya Al-asri. Maulidi huanzia msikiti
wa Jumaa na kuandamana kupitia baharini dhefe husimama katika Msikiti wa Shella
wakaombea wafu dua. Wakitoka hapo wanakwenda msikiti wa Biniamuni-sasa “Masjid
Qubaa” hapa pia husimama wa kuombea wafu dua katika maziara hapo kwa msikiti kwa
Biniamuni:
Kutoka hapo dhefe ambazo zina fika karibu ishirini
hutoka madrasa tafauti tafauti kama vile kutoka madrasa za Malindi, Mambrui Kakunyeini,
Takaungu na kwenginepo. Kila madrasa huwa zina imba qasida tafauti na kwenda mrama
huku wakitafautiana huku wakipiga matwari
na vigoma . Maulidi haina tarumbeta au zumari.
Qasida husomwa kwa mahadhi mazuri ya kuvutia .
Katika maulidi makubwa ya Malindi Mambrui, na Kipini
mara nyingi kupatikana Ngoma ya shabuwani, wakati wa zamani huwa na mashindano ya
shabuwani baina ya Malindi, Mombasa na Mamburui. Mashindano haya hufanywa siku
ya Maulidi makubwa ya kila mwaka.
PREPARED BY
ABUD SALIM MBARAK BAZMALEH
WINNER OF SPECIAL CATEGORY, HUMAN RIGHTS AWARD, 2006
+254 -724338113
SUBMITTED TO DORIS KAMUYE
MALINDI MUSEUM – WEBB MEMORIAL LIBRARY