Friday 3 August 2012

Mti wa Muhina.....

Abdi Ahmed, 12 Years. 5 East. Mombasa Primary School.

Muhina ni mti unaotoka Yemen, nyanya alituelezea.Ni mti kiasi na ukikuwa una majani mengi sana. Mti huu humea mwituni lakini pia watu wa zamani bado wanaupanda uani mwao. Muhina hutundwa majani  kisha ukachungwa na kutiwa ndani ya madebe kasha kisha kupelekwa kwenye mji kuuzwa.  Watu hununua kwa kipimo kulingana na matumizi. Unga wa hina hutiwa ndani ya bakuli ukaongezwa chai ya rangi na ndimu kasha kupaka.  Heena nyanya alielezea kuwa yatoka India na Egypt.
Heena ni mapambo inayotumika na wanawake wanapo olewa na wanapoudhuria sherehe ya harusi. Watoto wa kike hawaruhusiwi kupaka ila wakati wa sherehe ya Iddi. Nyanya  alisema heena ipo tangu jadi sana ikitumika upande wa bara Rabu, India na Egypt kwa kujipamba, lakini hapa kwetu pia hutumika kama dawa yakupoza presha ikiwa juu, mti wa mgongo, miguu na pia nywele kwa watu wazima kubadilisha rangi za nywele zao. Katika sherehe zetu za waswahili tuko na heena party. Bwana harusi hufinikwa na kitambaa na kupakwa heena kwenye mikono yote na mwili.



1 comment:

  1. useful knowledge that lots of people do not know. Thanks to Elimu asilia

    ReplyDelete