Amira Msallem |
Somo
Kiswahili huwa ni khalati/shangazi wa mtoto wa kike. Mtoto wa kike anapofika miaka kumi na nne au
tano hivi huvunda ungo.
Kuvunda ungo ni kubaleikh au kupata hedhi kwa mara
ya kwanza. Kunao uwezakano kwa mtoto wa
kike kuvunda ungo mapema kuanzia miaka tisa na vile vile kuna wale huchelewa. Haya yote hutegemea:
·
Kizazi ya familia
·
Mazingara yaweza kusababisha kupata hedhi mapema
ama kuchelewa kwa mtoto wa kike.
·
Vyakula huchangia pakubwa pia
Yote tisa, kumi kuvunda ungo kwa mtoto wakike na
furaha kubwa sana khaswa khaswa kwa mama mzazi.
Kwani mtoto wa kike anapo baleikhe ama kuvunda ungo, huwa ni ishara
nzuri:
·
Yaonesha kuwa amekamilika kuwa mwanamke
·
Amevuka daraja na kupanda cheo kwani sasa ana
julikana kama Mwari/Mwanamwali
·
Ni ishara kuwa sasa anaweza kutafutiwa mchumba,
amekamilika kuwa mke nyumbani.
Pindi tu, anapovunda ungo mtoto wa kike mara ya
kwanza, mtoto yule hupelekwa kwa khalati/Shangazi yake ama ukipenda (SOMO) kupata
elimu muhimu ya;
·
Dini
·
Mila na desturi
·
Usafi wa mwili wake na nguo zake
DINI:
Dini ni muhimu sana na pia nimuongozo bora. Mtoto wa kiislamu akiinukia tayari hufundishwa
dini ama hukuwa na dini lakini hata
hivyo pindi mtoto wa kike anapo baleikh ama kuvunda ungo somo humfundisha tena
kuhusu dini na hedhi kwa urefu na kwa njia njia yakufahamika . Khaswa mambo ya muhimu na lazima kwa mtoto wa
kike kama:
·
Umuhimu ya hijabu kwa mtoto wa kike
·
Mavazi ya sitara na heshima
·
Sheria ya dini unapokuwa kwa hedhi na namna yakujitwahirisha
·
Mwari au mwanamali haruhusiwi kukurubiana na mtoto
wa kiume
·
Usafi na umuhimu yake kwa mwanamwali wa kiislamu.
MILA NA DESTURI:
Mbali na dini mila na desturi ni muhimu kwa mtoto
wa kike, kwa sababu baada ya kubaleikh huwa kuna uwezakano ya kuolewa kwa
haraka kama desturi ilivyo bila ya kupoteza wakati, naiwapo mwari/mwanamwali
atakuwa hajui mila na desturi huwa ni aibu kubwa kwa wazee wake na familia.
Somo yake mtoto huchukuwa jukumu nakuakikisha kwamba Yule mwanamali ana jua
mila na desturi. Mtoto yule wa kike
atafundishwa na somo :
·
Kuingia jikoni afundishwe kupika kwa ustadi na namna ya kuandaa mankuli.
·
Heshima na adabu njema kwa wazee, wanaomshinda kwa
umri
·
Mtoto wa kike hafai kucheka kwa sauti ya juu ama
kuzungumza
·
Mtoto wa kike hufundishwa kuwa na haya na khaswa
anapozungumza na watu wazima wake ni sharti
azungumze kwa sauti ya chini na unyenyekevu na adabu
·
Mtoto wa kike anapo baleikh hufundishwa kujisitiri
na kuwa mustarabu, anapoketi chini panapo watu wazima akae kwa heshima,
anapolala, atakiwa kulala kitumbo tumbo
·
Avae mavazi ya sitara na heshima
·
Awe ni maridadi wa mwili wake, umaridadi wa usafi
na umaridadi wa akili na kuwa na busara.
Haya yote niliotaja ni baadhi tuu, ya mafundisho
na matayarisho kwa mtoto wa kike anapo baleikh au anapo vunda ungo .
MTOTO WA KIKE ANAPOVUNDA UNGO MARA YAKWANZA AU
ANAPO BALEIKH
Mtoto wa kike anapovunda ungo mara ya kwanza au
kubalekh hupelekwa kwa shangazi/khalati
(SOMO) kwa mda ya wiki mbili kuelimishwa elimu mbali mbali yanayopasa mwanamke
kujua , kisha mwari Yule huregeshwa nyumbani kwa mamake mzazi akiwa na elimu
yakutosha kumsitiri , akili huwa ya kiutu uzima, huwa amebadilika kwa tabia na
ujihisi amepanda daraja au cheo nyingine katika maishani mwake.
Mwanamwali Yule huregeshwa kwa somo pindi tuu
akiingia kwenye hedhi tena kwa mara ya pili, lakini tofauti na awali ama mara
ya kwanza safari hii ya pili huwa ni
kama mtihani. Somo ataka kuangalia jee aliyofunzwa mwari alishika? Au amefaulu
? lau atakuwa ameshika aliyefunzwa na somo wake basi akimaliza hedhi yake mwari
huregeshwa nyumbani kwa kwao na zawadi ya leso gora mbili, mmoja huvaa na
nyingine akakibeba.
Baada ya hapa somo hana kazi tena mpaka siku ya
kuolewa mwari wake.
SOMO –
KHALATI/SHANGAZI
KWA MTOTO
WA KIKE ALIYE VUNDA UNGO AU KUBLEIKH
WA
KISWAHILI
NA
AMIRA
MSALLEM
No comments:
Post a Comment