Abdi Ahmed, 12 Years. 5 East. Mombasa Primary School. |
Muhina ni mti unaotoka Yemen, nyanya alituelezea.Ni mti kiasi na ukikuwa
una majani mengi sana. Mti huu humea mwituni lakini pia watu wa zamani bado
wanaupanda uani mwao. Muhina hutundwa majani
kisha ukachungwa na kutiwa ndani ya madebe kasha kisha kupelekwa kwenye
mji kuuzwa. Watu hununua kwa kipimo
kulingana na matumizi. Unga wa hina hutiwa ndani ya bakuli ukaongezwa chai ya
rangi na ndimu kasha kupaka. Heena nyanya
alielezea kuwa yatoka India na Egypt.
Heena ni mapambo inayotumika na wanawake wanapo olewa na wanapoudhuria
sherehe ya harusi. Watoto wa kike hawaruhusiwi kupaka ila wakati wa sherehe ya
Iddi. Nyanya alisema heena ipo tangu
jadi sana ikitumika upande wa bara Rabu, India na Egypt kwa kujipamba, lakini
hapa kwetu pia hutumika kama dawa yakupoza presha ikiwa juu, mti wa mgongo,
miguu na pia nywele kwa watu wazima kubadilisha rangi za nywele zao. Katika
sherehe zetu za waswahili tuko na heena party. Bwana harusi hufinikwa na
kitambaa na kupakwa heena kwenye mikono yote na mwili.
useful knowledge that lots of people do not know. Thanks to Elimu asilia
ReplyDelete