FASTING DURING THE MONTH OF RAMADHAN
The 5 pillars of Islamic faith
SAWM
Mohammed |
MAPISHI USWAHILINI.
MAPISHI USWAHILINI KATIKA SIKU YA IDDI
MAANDALIZI
Maankuli ya siku kuu huandaliwa
siku ya mwisho ya ramadhan. Vyakula hivi haswa ni vyakula visivyo vunda na
huweza kutoharibika kwa muda wa wiki. Upishi huu huwa ni wa ustadi na taaluma
ya uswahilini na kiarabu.vyakula zaidi ya aina tatu huandawa na akina mama. Ni
jukumu la kiongozi wa nyumba ambaye haswa ni baba kuhakikisha maakuli ya siku
ya iddi yako tayari.
AINA YA VYAKULA VYA IDDI
Mkate wa sinia
Mkate wa tambi.
Mkate wa mayai
Kokoto
Sambusa
Bokoboko
Halua
Vishete
Donasi
AINA YA MASHARUBETI
Kahawa chungu
Chai ya maziwa
Milk shake
Vinywaji vya matunda
Vyakula hivi ni vya kushilikiza
tumbo, kwa kingereza huitwa”bites”, kwa maana haipaswi mtu ale mpaka ashibe. Kwa
hivyo ale kwa uchache tu. Mapishi ya vyakula hivi ya kiwa tayari, huandawa
mezani. Vyakula huandaliwa mezani pindi wanaume wakiwa msikitini katika swala
ya iddi. Baada ya swala ya iddi, vyakula huwa tayari vimetapaka mezani. Wanaume
na watoto huingia majumbani katika matembezi ya aila zao. Katika matembezi haya
ndipo hukaribishwa mgeni kwa vyakula hivi.
MAPISHI USWAHILINI KATIKA SIKU ZA RAMADHAN
Maankuli katika siku za ramadhan huwa vimegawanyika katika sehemu
tatu. Sehemu hizi ni:
- Chakula cha kufungulia mwadhini
- Chakula cha futari
- Chakula cha daku
CHAKULA CHA KUFUNGULIA MWADHINI
Upishi wa vyakula hivi huwa ni wa
kwanza kabla ya vyakula vingine kupikwa.Vyakula hivi huwa havipikwi kwa wingi
lakini hupikwa kwa uchache wa idadi ya watu pale nyumbani.Vyakula hivi ni kama:
v
Viazi vya kukaanga
v
Bajia
v
Kaimati
v
Katlesi na kababu.
v
Vinywaji pia ni muhimu kupatikana haswa vinywaji vya matunda
Katika majumba mengine vyakula
hivi hupikwa kwa wingi na hupelekwa msikitini kwa wale walio msikitini kufungua
mwadhini hapo.
CHAKULA CHA FUTARI.
Upishi huu ni wa pili. Chakula
hiki hupikwa kwa wingi kwa kutosheleza watu wote mle nyumbani na mgeni yeyote
atakae kuja. Vyakula hivi huenda vikagawanyika katika mafungu mawili.Nayo ni:
CHAKULA KITAMU.
Katika futari chakula hiki huliwa
mwanzo .Vyakula hivi huwa vinapikwa kutumia sukari nyingi hadi kuleta ule utamu
wa chakula chenyewe.mifano ya vyakula hivi ni:
Viazi vitamu.
Tambi za mapapai.
Matangu.
Matobosha.
Vibibi.
Mabatali
Ndizi za kiume
Makoranya ya sukari.
Pojo.
CHAKULA CHA CHUMVI
Katika futari, chakula hiki
huliwa mwisho.vyakula hivi hupikwa kwa kutumia chumvi katika upishi wake.Mifano
ya vya kula hivi ni:
- Mihogo ya nazi.
- Chapati
- Viazi vya nazi
- Mkate wa fushi
- Mkate wa mofa kwa nyama.
- Viazi vya rojo.
Kabla ya kula vyakula hivi
waswahili hunywa kinywaji maaruf kinachoitwa”shurba”. Kinywaji hiki ni cha uji
wa ngano, mtele, nyama na bizari ya pilau. Mwisho wa kula vyakula hivi,waswahili
hula/hunywa podini,kastadi au fahida.
CHAKULA CHA DAKU
Chakula hiki ni cha mwisho
kuandaliwa baada ya vyakula vyote kuandawa. Vyakula hivi haswa ni vya
carbohydrates na protini. Waswahili hula wali na mchuzi wa viazi kama daku lao.
Daku huliwa saa tisa hadi saa kumi za usiku. Baada ya saa kumi ndipo saumu
inapo anza na si ruhusa kwa mwislamu yeyote kula chakula chochote.
BEMBE
Chakula hiki huliwa katika saa
tano au sita kabla ya watu kulala.Vyakula hivi haswa ni vya nyama.kwa
mfano:supu ya nyama ama nyama ya kuchomwa na chipsi
No comments:
Post a Comment